spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers
spacers home the model find a video Product spacer
spacer Help search Sitemap about
line

Kitovu cha mafunzo binafsi ya wanafunzi

 

    

Hitimisho

Tafsiri

Orodha ya tabia zinazoweza kuonekana

Mfano

 

Mfano

Asili ya kujifunza 

Ili kuwasaidia wanafunzi wa daraja la tano na la sita katika kuelewa wazo kuhusu mbinu za kuishi kama inavyohusika katika ulimwengua wa wanadamu na wanyama, wanafunzi hujiundia tafsiri ya maana ya kuishi pamoja na kuyazoea mazingira. Kuhusiana na ufahamu huu badaye wanaunda simulizi yenye ujumbe unaohusu kuishi. Wanafunzi pia wanatafiti njia amabzo wanyama wanaisha kwa kuyazoez mazingira yao mapya katika sehemu kama za ncha ya kaskazini na kusini mwa dunia, jangwani, misituni, savana, na sehemu za milima. Wanyama wanakuwa wamehitimisha kipengele cha mwongozo wa kuishi kama makazi yao, shule, katika maisha ya jamii kwa ujumla. 

Rejeo

      Forte,  I.,  &  Schurr,  S.  (1994).   Interdisciplinary units and projects for thematic instruction.  Nashville, TN: Incentive Publications.

Malengo ya kujifunza 

Lengo la msingi la shughuli hii kwa wanafunzi wa daraja la nane ni kuchunguza vipengele kadhaa vya mila na desturi za wamarekani vilivyochaguliwa kwa kipindi kirefu sasa ili kufumbua vipaji, tamaduni, na alama za kuendela kukua kwa mafanikio. Ili kufanya hivyo wnaafunzi wajihusisha katika shughuli zifuatazo:kuchungua zana za awali wakatika wa Marekani ya kikoloni., kugundua jinsi kingereza cha mitaani yaani slang kilivoanza kufuatia matukio ya kihistoria, kutafiti juu ya mashujaa wa kimarekani wanaowataka wenyewe, na kisha kuwasilimua habari zao: na kukusana nukuu katoka katika historia na kuzitafsiri maana yake. 

Rejeo 

      Forte, I., & Schurr, S. (1994).   Interdisciplinary units and projects for thematic instruction. Nashville, TN: Incentive Publications.  

Uundaji wa ujuzi 

Katika darasa la hesabu la wanafunzi wa daraja la nne walimu anawasaidia wanfunzi kuunganisha habari mpya na zili ambazo tayari wanazifuhamu. Hatua ya kwanzi ni kupitia masomo awali ambayo yanaweza kuwasaidia wanafunzi kukumbuka habari zitakazowasaidika kuelewa vitabu wanavyojifunzia. Kwa mfano mwalimu anaweza kuuliza, “nani anaweza kutupa tafsiri ya neno ‘quadrilateral’? ni umbo la mraba, tulisema nini jana kuhusu jinsi ya kulitambua? Leo tutaangalia kuhusu maumbo mengine. 

Rejeo

      Woolfolk, A. (2001).  Educational psychology (8th ed.).  Needham Heights, MA: Allyn & Bacon.

Kiwango cha juu cha kufikiri 

Lengo la zoezi hili ni kukuza ujuzi wa wanafunzi katika kutatua matatizo na kufanya maamuzi katika daraja la tisa na la kumi. Zoezi linatumia mfano halisi wa mahali pa kufanyia mannunuzi au dukani ili kuweza kutumia mahesabu mbalimbali na mbinu za ununuzi. Kwa kuwa vijana wantumia muda wao mwingi katika maduka, ina kuwa jambo lenye maana kutumia mfano huu katika kuchunguza mawazo ya kimahesabu katika mazingira halisi ya kiulimwengu. 

Malengo maalumu ni pamoja na: 

 1. wanafunzi wanaangalia watu wanaonunua wakiingia na kutoka madukani na hatimaye wanafanya hitimisho kuhusiana na utaratibu wa kutembea wa msongamano wa watu wanaopendelea. 

 2. Wanafunzi wapima plani na ukubwa wa nafasi na kisha kutoa uamuzi kuwa na duka lipi lina asilimia kubwa ya nafasi katika duka.

 3. Wanafunzi wanachambua uwiano kati ya maduka yanayouza vitu na yale yanayotoa huduma kwa watu.

 4. Mwanafunzi anagundua njia ambazo wauzaji wanazitumia katika kuwavutia wateja ili kununua katika maduka yao.

 5. Mwanfunzi anabuni mfano halisi wa maduka kwa ajili ya watoto kulingana na mahitaji yao pekee. 

 6. Manfunzi anapanga bajeti ya chakula kwa siku na kulinganisha thamani ya ununuzi wa bora kinachopatikana madukani (Forte & Schurr, 1994, p. 150).   

Rejeo

      Forte, I., & Schurr, S. (1994).   Interdisciplinary units and projects for thematic instruction. Nashville, TN: Incentive Publications.

Vihamasisho wakati wa kujifunza 

Wanafunzi wanaanisha

Wanafunzi wanaainisha ni nani kati yao ambao wana ujuzi au ufahamu zaidi kutokana na majaribio wanayopewa katika zoezi hili hasa wanafunzi wa madaraja ya sita na saba kwa kuuliza Nani ajua kutumia komputa katika kufanya michoro? Jinsi ya kutumia mtandao wa intaneti? namna ya kutumia faharasi? Wanafunzi wanaojitokeza wanapaswa kuwasaidia wenzao ili kuwawezesha kupata ujuzi ambao tayari wao wanaujua (woolfolk, 2001,p.354). 

Rejeo

      Woolfolk, A. (2001).  Educational psychology (8th ed.).   Needham Heights, MA: Allyn & Bacon.

 

Vihamasisho vihusishi katika kujifunza 

Zoezi hili limebuniwa ili kuhisianisha malengo na uzoefu wa wanafunzi. Kwa mfano, wanafunzi katika shule ileile wanaweza kuanza kuandikiana wao kwa wao kati ya darassa na darasa. “Kwa njia ya kuandikiana barua wanaweza kubadilishana uzoefu katika mambo waliyoyapitia, picha, michoro, kazi zilizoandikwa, kuliza na kupeana majibu katika maswali mbalimbali (‘vitabu gani unavyopendelea zaidi kuvisoma?, kwa nini? Vipi maendeleo yako katika hisanati hivi sasa?’)”. (Woolfolk, 2001, p. 367). 

Rejeo

           Woolfolk, A. (2001).  Educational psychology (8th ed.).  Needham Heights, MA: Allyn & Bacon.

 

Characteristics of motivation-enhancing learning tasks

Tabia za vihamasisho vinavyofanikisha nyajibu za kujifunza Kukuza hamasa asili na tabia ya kisomi katika kufikiri juu ya wakati ujao kwa wanafunzi wa madaraja ya kati, pia kujaribu kuwawezesha kumaliza mafunzo ya awali juu ya mambo ya mbeleni kwa wanafunzi katika somo la jiografia. Wambie wanafunzi wajifanye kuwa vyombo vya angani sita vilirushwa kutoka katika sayari tofauti. Lengo lake ni kutua katika sehemu zifuatazo: Disney world huko Florida; Beijig, China; Boston, Massachusetts; Athens, Ugiriki; Kairo, Misri, na Mto Amazoni nchini Brazil. Waambie wanafunzi wabuni majibu ya maswali yafuatayo: 

 • Hali ya hewa ikoje?
   

 • Elezea juu ya milima na mabonde ya nchi. 

 • Je watu wa maeneo haya wanakula, wanavaa na wajishghulisha na nini? 

 • Ni mahali gani au matukio gani yalikuwa ya kufurahisha zaidi? 

 • Ni kitu gani ambacho si cha kawaida au ni cha kipekee katika sehemu hii? (Schurr, 1994, p.89).

Rejeo

            Schurr, S.  L.  (1994).  Dynamite in the classroom: A how-to handbook for teachers.  Columbus, OH: National Middle School Association.

Vikwazo katika kukua kwa viwango na mafanikio 

Wanafunzi wana mitindo tofauti katika kujifunza, na ndio maana wanafunzi wanajitahidi kutafuta mazoezi mbalimbali yanayowafaa wanafunzi mabalimbali. Kwa mfano, kwa wanafunzi wa daraja la tano na sita wanaojifunza kuhusu mazoezi na mijongeo ya mwili, mwalimu wao anaweza kuwaambia warekodi mapigo ya moyo. Wanafunzi wanaweza kuelekezwa kufanya mijongeo mbalimbali na wengine kulegeza maungo kwa kujilaza chini au kusimama majali pamoja. Kisha wanafunzi wanaweza kulinganisha kasi ya mapigo ya moyo kati ya wale ambao walikuwa wakijongea na wale waliokuwa
wamesimama mahali pamoja ili kuwa na ufahamu mzuri wa namna moyo unavyofanya kazi. 

Tofauti ya kijamii na kiutamaduni 

Katika zoezi hili ambalo ni kwa wanafunzi wa daraja la nane, wanafunzi wanajifunza kuwa “miduara inayopandana katika hisabati inaitwa michoro ya Venn. Michoro ya Venn inatumika katika kuonesha
kufanana na kutofautiana kati ya watu wawili au zaidi, mahali au vitu. Sehemu ambapo michoro hii inaingiliana panaitwa mwingiliano au mkutano wa miduara (Intersection of the circles). Sehemu hii inaonesha kitu ambacho watu, mahali au vitu vinafanana” (Forte & Schurr, 1994, p.178). 

Mwalimu awaambie wanafunzi wachore miduara miwili inayoingiliana inayowakilisha wao na rafiki zaowapedwa. Katika eneo lisiloingiliana la mduara, wanafunzi waandike mambo yanayowafanya wao kuonekana tofauti na rafiki zao, katika duara michoro inapoingiliana waandike namna wanavyofanana na rafiki zao. Wanfunzi wanaweza kufanya hivyo kwa kuzingatia vitu kama maumbile, tabia, na jamii wanakotoka pamoja na vitu binafsi wanvyopendelea au wanavyofurahisha. 

Halafu, wanafunzi wachore duara la tatu ambalo linapandana na zile mbili za awali ambalo linasimama badala ya umoja katika urafiki na wanafunzi wawili wa awali. Katika mwingiliano wa miduara, waandike vitu ambavyo wote watatu wanafanana. Mwalimu awaambie wanafunzi kuonezea mwanafunzi wa nne na wa tano kwenye mchoro huu na kuonesha namna mchoro utakavyofanya kazi. 

Rejeo

     Forte, I.,  &  Schurr,  S.  (1994).  Interdisciplinary units and projects for thematic instruction, p. 178.  Nashville, TN: Incentive Publications.

 

Kukubalika kijamii, hisia binafsi na kujifunza 

Mwalimu aandae darasa la wanfunzi wa daraja la nane kuwa kama jamii ndogo, atoe huduma zote ambazo jamii yoyote ingekuwa nazo. Mwalimu aunde baraza la serikali ambalo linajumuisha meya na wawakilishi katika baraza. 

Darasa lichague meya mwingine na wawakilishi wa baraza ambao kila moja linawakilisha muhula mmoja. Darasa liwa limegawanyika katika vikundi vinne, na kila kundi lichagu mjumbe wa baraza. Makundi ya wanafunzi yakae pamoja mezani au kwenye mkusanyiko wa madawati. Wajumbe wa baraza wakutane na meya ili kuweka sheria za darasa, faini pamoja na kupanga mambo ya jumuiya na kujadili matatizo ya jumuiya. 

Rejeo

     Forte, I., & Schurr, S.  (1994).  Interdisciplinary units and projects for thematic instruction, p. 42.  Nashville, TN: Incentive Publications.  

Tofauti za kila mtu katika kujifunza 

Wanafunzi wanaopendelea kufanya shughuli peke yao wana hamasisha ukuaji“binafi wa akili” (Gardner, 1999). Shughuli inayofaa kwa wanafunzi wa aina hii katika madaraja ya nane na tisa ni kuwafanya wajifunze mbinu za uandishi wa barua kwa kupita tukio linalotokana na uamuzi fulani. Shughuli hii inaweza kutumika darasani wakati wa vipindi au kama kipimo cha kuwahimiza wanafunzi wakuze ujuzi kwa ajili ya mafanikio yao wenyewe. Katika zoezi hili mwalimu anaweza kufanya yafuatayo. 

 • Awaoneshe wanfunzi mfano wa barua kwenye kiwambo au mwalimu anaweza kuwapa kila mwanafunzi nakala ya barua aliyoichagua. 

 • Kupitia kila kipengela na mfumo mzima wa barua (kama vile anuani, tarehe, na salaamu/utangulizi) pamoja na vigezo vya barua fasaha ( kama vile fasihi, na kadhalika)

 • Wanafunzi waandike barua ya kurasa mbili kwa rafiki zao kuhusu jambo falani muhimu waliloamua

 • Mwalimu apitie na kuona hilo linavyofanyika.

Kama darasa au kikundi kidogo, wanafunzi wanchangie mawazo mablaimbali na kuamua juu ya vichwa fulani vya habari “. (Bellanca, 1977, p. 42). 

Rejeo

            Bellanca, J. (1997).   Active learning handbook for the multiple intelligences classroom.  Arlington Heights, IL: IRI/ SkyLight Training and Publishing.

            Gardner, H.(1999). Intelligence reframed: Multiple intelligences for the 21st century.  New York:  Basic Books.                                                                                                                        

Mchujo wa kiuelewa 

Zoezi hili linawasaidia wanafunzi wa vidato vya juu katika kutambua dhania na matokeo yanayoambatana na dhania hizo katika fikra za wanafunzi. Mwalimu awaambie wanafunzi waandike katika kumbukumbu zao wazo kuhusu umuhimu wa kulala katika maisha yao, na kiwango cha sukari wanachotumia kila siku. Baada ya zoezi hili fupi, mwalimu amkaribishe mganga kama mgeni na msemaji maalumu wa siku hiyo. Mganga azungumzie madhara ya ya kutokuwa na usingizi wa kutosha na hatari ya kuwa na kiwango kikubwa cha sukari katika mmaisha ya wanafunzi. 

Mwishoni mwa darasa mwalimu awape wanafunzi zoezi la kuandika katika kumbukumbu zao mawazo ya juu ya usingizi na sukari mwilini. Hii inaweza kuwapa wanafunzi nafasi ya kubadikika katika uelewa wao kwa kutambua matumizi ya sukari na kupata usingizi kwa mtazamo mpya. 

Rejeo

     Callahan, W., & Cimpoeru, C.  (2000).  Cognitive filters example.  Unpublished manuscript.  

Mafundisho yanayolenga wanafunzi 

Mwalimu ya darasa la tisa anahitaji wanafunzi kufanya mafaribio ya vitu mbali mbali kwanza huwaonyesha mizani ya saa rahisi na kuelezea inabembea mara ngapi kwa kipindi cha mda fulani. Anawaambia wanafunzi kutoa mfano ya kawaida na wanafunzi wanatoa mzani ya saa na mishale. Mwalimu anawauliza kuwa ni vitu gani vinavyo weza kudhuri uwengi wa kubembea kwa mshale. Wanafunzi wanatoa majibu kuwa ni uzito, ulefu, na pembe mshale unapoanzia . 

Mwalimu huwapa wanafunzi maelekeo ya kubuni maelekezo ya kubuni majaribio yao wenyewe kuhusu ni kwa vipi vituhivyo vinashuru mbembeo wa mshale. Anaunda makundi ya wanafunzi wane na kuwaambia kufanya majaribio katika vikundi. 

Wanafunzi anafunga uzi kwenye kitasa na kupima urefu wake. Mwanafunzi mmoja wapo anapoma urefu wa uzi wakati mwingine anarekodi urefu huo. Kama kikundi wanajadili jinsi ya kuendelea. Wanafikiria mlingano watakayo weza kutumia kutafuta vitu vinavyo sababisha madhara katika jaribio. Wanafanya kazi kwa pamoja wakiongoza kujifunza kwao. Kwa kutumia rula kupima mshale wa saa na kadri unavyo bembea wakati uzi ukiwa na urefu tofauti. 

Katika jaribio la pili wanafunzi kuongeza kikaratasi kwenye uzi ili kuufanya uwe mzito kidogo. Katika jaribio la tatu, wanafanya jaribio kupitia pembe tofauti ambao mshale unaanzia. Wanakusanya majibu baada ya kila jaribio. Wanafunzi wanakuwa wamahusishwa katika shughuri halisi zinazo wawezesha kuelewa mfumo mzima wa mazala ya majaribio yao. Walimu huongoza kazi ya wanafunzi lakini hafanyi kazi nao. Wanafunzi wanawajibika katika kujifunza kwao.

Rejeo

            Eggen, P.,  &  Kauchak,  D.  (1999).  Windows on classrooms (4th ed.).  Upper Saddle River, NJ: Merrill.