spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers spacers
spacers home the model find a video Product spacer
spacer Help search Sitemap about
line

 

Matafakari

 

    

Tafsiri

Mtafakari ni mfumo wa akili unaoshughulikia jinsi ya kujifunza na hutatanisha wanafunzi kujumia uwezo wao wa kufikiri kwa kiwango cha juu kuchanganua habari, kujua uhalali wake, na kutoa hitimisho kutokana na mawazo yaliyokusanywa. Mfumo huu unaoendelea uanawaruhusu wanafunzi kutoa majibu yao na kufikia tamati. Matiokeo ya kufikiria huko kunafananya wajifunze na kuweza kufaulu katika kuelewa fikra mbalimbali. Bila kutafakari, kujifunza huwa kidogo sana na hukosa ujifunzi wa undani zaidi kama inavyotakiwa na mapangilio wa kufikiri” (Ewell 1997b, p. 9). Kujifunza kwa usahihi unahitaji muda wa kufikiri. Wanafunzi pia hujifunza jinzi ya kutathmini yale waliojifunza na mifumo ya kufikiri kwao ili kutafuta mbinu zinazofaa zaidi. Wanaweza kutumia habari wanayopata kwa kujifunza siku za mbeleni.             

Kaguo ya Orodha ya Tabia Zinazoonekana

___ 1. Akili nyingi (Donovan, Bransford, & Pellergino, 1999, p. 14): 
           Haya mazungumzo ya ndani kwa ndani huwafanya kuongoza
           kujifunza kwao na huwasaidia kujenga mbinu za kutabiri
           majifunzo na matokeo na kuangangalia mipango mizima ya 
           uelewa.

___ 2. Kusafirisha na kupokea Elimu (Donovan, 1999, p. 6) 
           Wanafunzi hupanua walio jifunza katika mazingira ya zamani
            katika mazingira mapya.

___ 3. Kufikiri kwa kutumia mifano (Donovan, 1999, p. 13):
           Wanafunzi hulinganisha na kutofautisha ujuzi wao na mambo
           wanayoyafahamu ili kutafuta maana na majibu yanafaa katika
           mazingira fulani.

Marejeo

          Donovan, S., Bransford, J., & Pellegrino, J. (Eds). (1999). How people learn: Bridging research and practice. National Academy of Sciences [On-line]. Available: http://bob.nap.edu/html/howpeople2/

            Ewell,  P.  T.  (1997).  Organizing for learning: A point of entry.  Draft prepared for discussion at the 1997 AAHE Summer Academy at Snowbird.  National Center for Higher Education Management Systems (NCHEMS). Available: http://www.intime.uni.edu/model/learning/learn_summary.html

Mfano                                                                                     

“Kusherehekea hali ya utabaka katika Shule za Iowa” ni somo la jamii kwa wanafunzi wanaoitwa Junior na Senior katika kitato cha juu kuwapa uzofu wa mila na desturi zaidi ya wanayoyapata chuleni, kusheherekea utabaka Iowa, na kujifumza jinsi ya kujifunza , kuelekeza, makundi makubwa ya mikutano. Kwa mradi wao wa mwisho wa somo, wanafunzi wanfanya utafiti, watapanga, na kuelekeza, ICN (Chombo cha Mawasiliano cha Iowa-Iowa Communication Network) mikutano ya Matabaka ambapo wanafunzi wengi toka katika jimbo/mmkoa wa Iowa huja na kushiriki katika kupeana mawazo kuhusu mambo ya mila mbalimbali, fikra, na mawazoili kusheherekea utabaka kama sikukuu maalumu inayowahusu watu wote. Somo hili linawahusu wanafunzi kuwa na uwezo wa kujifunza na kutafakari kutoakana na uzoefu wao wa awali ambao walikumbana katika mila zao na desturi.

Katka kuandaa darasa, mwalimu ataongoza mjadala unaohusu kutafakari na kutaka kupata mawazo mbalimbali kuhusu matabaka, ili kupata mawazo ya wanafunzi na jinsi mawazo haya yanavyobadilika kwawakati huu. Wanafunzi watajadili tofauti katika mila, dini, jamii, imani, makabiala, maisha ya mjini na tofauti yake na maisha ya kijijini, migongano ndani ya tabaka, jinzi vyombo vy habari vinavyosema kuhusu matabaka, hasa ni nini kibaya na ni nini kizuri, upendeleo, uelewa wa awali, na tabia inayojitokeza katika maeneo mbalimbali.

Mwalimu anawauliza wanafunzi kubadilishana mawazo kuhusu jinsi walivyosafiri na kukutana na hali hiyo katika miji mikubwa na midogo na miji mingine ya ulaya. Katika mfumo huu, utafakari hutokea mara kwa mara wakati wanafunzi wanapoambiana hadithi zao. Wanafunzi huulizwa kuhusi ni kiasi gani waliogopa na jinsi walivyokabiliana n ahali hiyo hasa katika mazingira yenye mila na desturi mpya. Katika mfumo huu, mwalimu huwauliza wazo lao la kiujumla lilivyojadiliwa kuhusu mila na desturi na tabaka katika mazingira fulanim, kama vile mila na desturi za Iowa na kutakari kuhusianisha na mila za shule kwa kiujumla.

Rejeo

            Pralle,  S.  (2000).  Celebrating diversity in Iowa schools [Video].  INTIME: Integrating New Technology Into the Methods of Education. [On-line].  Available: http://www.intime.uni.edu