Ufundishaji mzuri unatokana na kufanya uchaguzi mgumu wa kisheria, kufanya mazoezi ya maamuzi kwa uangalifu, na kutukuza malengo mchanganyiko ya asili ya kielimu. Licha ya ujuzi wa kitekinolojia na mbinu za waalimu amabazo wanahitajiwa kutumia kila siku wanapofundisha, wanatakiwa pia wawe wanafahamu sheria za kiutendaji kazi za kiualimu. Kwa mfumo huu, kusudi la kwanza ni kuleta maendeleo ya ujuzi, muelekeo, na kuelewa, wakati ukitambulisha kwa makini na kwa kuwajibika mahitaji na hali mbalimbali za binaadamu. Kwa hiyo waalimu wanahitaji kuwa na ujuzi na mbinu nyingi za kiufundishaji, na kubaki katika hali ya uhakika, kukosoa, na kutafakari mbinu zao za kufundisha. Majukumu yao ya kazi yanalenga katika kuwafundisha wanafunzi, licha ya kushiriki katika shughuli nyingi shuleni na wanaposhirikiana na wazazi na jamii nzima.
Kutokana na maendeleo ya hivi karibuni ya umbinu za ufundishaji, kufundisha kumekuwa ni zaidi ya shughuli za kufundisha tu ambayo ina tunza elimu na elimu zinaothaminiwa kwa zinazorithishwa kwa vizazi vinachofuata. Kwa hiyo waalimu wanahitajiwa kupinga muundo uliopo, mazoezi, na maana ya elimu; kugundua na kujaribu mbinu mpya; na panapohitajika, na siku zote kufuatalia mabadiliko ya kimipango katika kujaribu kuendeleza shule. Kama watumishi wa serikali katika demokrasia, wanalimu katika utendaji wao wanazungumzia kuhusu kutunza na kuendeleza jamii, na wanaanzisha na kuwahusisha wazalendo katika mazungumzo haya yanayoendelea.
Viwango vya utendaji kazi kinawakilisha makubaliano ya kiutendaji kazi katika sura ya sanaa na sayansi ya kufundisha (mbinu za ufundishaji) amabazo zinaainisha walimu waliofuzu katika nyanja mbalimbali. Hatua zinazochukuliwa na walimu huendeleza wanafunzi,, viwango hivi pia huunganisha ujuzi wa kufundisha, mbinu, mwelekeo, na kujitolea ambavyo vyote hivi huwafanya waalimu wafundishe kwa viwango vya juu. Viwango hivi vinazingatia misingi ya kifalsafa ambayo ina vigezo vitano vya
kiini:
- Wanafunzi hujitolea kwa wanafunzi na kujifunza kwao
- Walimu wanajua wanayoyafundisha na wana mbinu za kufundisha zinazostahili
- Waalimu wanawajibika kuangalia na kuongoza kujifunza kwa kwanafunzi
- Waalimu hufiri hatua kwa hatua kuhusu wanayofundisha na wanajifunza kutokana na uzoefu wao
- Walimu ni wanachama wa jamii ya kujifunza
Waalimu maarufu huonyesha mbinu zinazounda mitaala iliyobuniwa ili iweze kujengeka katika uelewa na ujuzi wa wanafunzi wa sasa na kuwaelekeza katika uwezo, elimu, fikra, na utendaji wa hali ya juu. Wanakadiria majibu yao kutokana na mapendleo na uwezo wa wanafunzi, kuunda shughuli kulingana na kiwango cha uelewa cha wanafunzi kutokana na alivyoyanena Vygotsky, kuhusu kujifunza na maendeleo. Zaidi ya hayo, wasomi hawa wanatumia mbinu nyingi za ufundishaji na vifaa vingi kulingana na uwezo mbalimbali wa wanafunzi na kuwapa kila mwanafunzi njia nyingi za kugundua mawazo, mbinu, na fikra. Wanajua jinsi ya kufundisha kama waelekezaji, makocha, modeli, watathmini, viongozi, na mawakili. Zaidi ya hayo, waalimu wanajua mbinu nyingi za kutumia michezo ya kuigiza mingi, mbinu za kuwaweka wanafunzi katika vikundi, na aina nyingi za mawasiliano na vifaa.
Waalimu huangalia na kutathmini wanafunzi katika maisha ya darasani ya kila siku. Wana mbinu nyingi za kukusanya na kutafsiri ushaidi mwingi wa kuwa tathmini ambapo kila mwanafunzi kwa mfuatano au mizani ya kujifunza na maendeleo. Wanajua kutoka kwenye kutathmini na kuelekea kwenye kutoa maamuzi kuhusu mitaala, kuunga mkono kijamii, nyenzo za ufundishaji, kuwaongezea wanafunzi imani ya kufaulu.
Waalimu wanajua na wanaheshimu tabaka la watu wengi, uthamani, lugha, familia za wanafunzi walikotoka, kutumia watu wa jamii na mazingira kama chanzo cha elimu, kuwashirikisha wazazi na familia kama watu muhimu katika kukua na maendelo wanafunzi.
Kila wakati unawasilisha na kutoa nafasi kwa walimu kupambana kwa makini na mapingano yote ya darasani. Ni watu wanaochanganua kwa kutumia mbinu za hali ya juu sana kama kuangalia mwanafunzi mmojammoja na mazingira mazima yanayoweza kuongoza maamuzi yao. Wanatafakari utendaji wao kwa kupitia maendeleo ya wanafunzi, kutafuta mashauri ya wenzao na wazazi, na kufikiri kuhusu uchaguzi na matokeo ya uchaguzi huo.
Masuala Matano ya Utimizaji wa Ufundishaji.
Bodi ya Taifa ya Viwango Vya Ufundishaji inalenga kuainisha na kutambua waalimu ambao wanawafanya wanafunzi wajifunze na wanaoonyesha hali ya juu ya ujuzi, mbinu, uwezo, na kujitolea unaoonyeshwa katika masuala haya matano.
Waalimu wanawajibika kujifunza kwa wanafunzi
Waalimu maarufu hujitolea kufanya elimu kuwepo kwa wanfunzi wote kutokana na imani zao kuwa wanafunzi wote wanaweza kujifunza. Kwa hiyo, wanawapa wanafunzi elimu sawa kwa kutambua tofauti zao. Zaidi ya hayo, wanafundisha kwa kuzingatia tofauti hizo pia kutokana na kuangalia na kujua mambo ambayo wanafunzi wananyapenda, uwezo, mbinu, elimu, na hali ya familia, mahusiano kati ya wanafunzi wenyewe.
Walimu waliofanikiwa wanaelewa jinsi wanafunzi wanavyokuwa na kujifunza. Kwa hiyo, wataalam hao hutumia nadharia zilizopo za kuelewa na akili katika kufundiasha kwao. Zaid ya hayo, wanaelewa ushawishi wa mazingira na mila katika tabia. Katika hali hii ya ujumla, waalimu huendelea uwezo wa akili wa mwanafunzi na heshima yao katika kujifunza. Kwa maana hiyo hiyo, uzalendo, na kuheshimu wenzao, mila, dini, na tofauti za kitabaka.
Waalimu wanafahamu wanyoyafundisha na wanazo mbinu zinazohitajiaka
Waalimu waliofanikiwa wanelewa vizuri sana wanafunzi wao wanaowafundisha na kuthamini njinsi elimu inavyoundwa, pangwa, unganishwa na masomo mengine, na inavyohusiana na hali halisi ya dunia kwa wanafunzi wao. Wakati wakiwakilisha busara ya pamoja za mila zetu na kutunza thamani ya ujuzi wa nidhamu, pia wanaendeleza uhakiki na uwezo wa uchanganuzi wa wanafunzi wao.
Waalimu maarufu wanaongoza elimu za mbinu za kufundisha zinazotumiwa kufunua masomo kwa wanafunzi. Wanafahamu wanafunzi wanayoyafikiria na elimu yao ya awali ambayo waalimu huja nayo na kuhusianisha na wanayofundishwa pamoja na mbinu na vyombo vya ufundishaji amabavyo kwa vyote vinaweza vikawasaidia katika kujifunza kwao. Zaidi ya hayo, wanaelewa na wanaweza kutatua ugumu amabao unaweza ukatokea wakati wa darasani na kurekebesha mazoa yao kama inavyotakiwa. Mkusanyiko wa mbinu hizo huwasaidia kuunda njia nyingi kuelekea kwenye ujuzi, kwa ujumla, na hasa kwa masomo wanayofundisha.
Waalimu wanawajibika kuongoza na kupanga kujifunza kwa wanafunzi
Waalimu waliofuzu huunda, hutajirisha, hutunza, na hubadilisha mazingira ya kujifunza, vifaa, na mbinu ili kuvutia na kuendeleza yale yanayopendelewa na wanafunzi na kutumia mda wa kujifunza vizuri sana. Pia hujishughulisha na kuwa fanya wanafunzi na watu wazima katika kuwasaidia katika ufundishaji wao na pia kuendeleza mazoezi yao pamoja na ujuzi wa wenzao na utalaam wao.
Waalimu maarufu huamuru mbinu mbalimbali za ufundishaji na kuzitumia kwa usahihi. Huongoza kujifunza kwa wanafunzi na mazingira kwa ujumla. Kwa hivyo, mafunzo yanakuwa yamepangwa na kutimizwa ili kuwawezesha wanafunzi na kutimiza malengo ya shule. Waalimu wanaweza kuweka malengo na sheria za kijamii za ushirikiano kati ya wanafunzi na kati y awanafunzi na waalimu. Zaoidi ya hayo, wanaelewa jinsi ya kuwashawishi wanafunzi ili wajifunze na jinsi ya kuendeleza mapendeleo yao hata wanapokuwa wanakabiliwa na kushidwa. Walimu waliofanikiwa hutathmini maendeleo ya mwanafunzi kila mmoja na pia darasa zima. Wanatumia mbinu nyingi na hueleza maendeleo ya wanafunzi kwa uwazi kwa wazazi wao.
Walimu wanafikiria hatua kwa hatua kuhusu utendaji wao na kujifunza kutolana na uzoefu wao.
Waalimu maarufu ni modeli ya watu waliosoma, ikitoa mfano wanaoitafuta kuwashawishi wanafunzi, uchunguzi, uvumilivu, unafuu, kuheshimu tofauti, kuthamini tofauti za ki mila. Wanatoa mifano ya uwezo unaohitajika katika kwa kukua kielimu—uwezo wa kufikiri na kuchukua mitazamo mingi, kuwa muundaji na kujitoa muhanga, kukubali jaribio na maelekezo ya utatuzi wa matatizo.
Waalimu waliofaulu hutoa elimu yao kutoka maendelo ya binaadamu, masomo na mafundisho, na uelewa wa wanafunzi kufanya maamuzi ya mazoezi ya kutosha. Maamuzi yao yapo sit u katika fasihi, ila katika mazoa yao pia. Wanajishughulisha katika kusoma kwa maisha yote na wanahitaji kuwapa moyo wanafunzi wao.
Kutafuta kuimarisha ufundishaji wao, waalimu maalum huangalia utendaji wao kwa makini, hutaka kupanua uelewa wao, kuimaridha ujuzi wao, kunoa maamuzi yao, na kubadili ufundishaji wao kutokana na utafiti, nadharia, na fikra
mpya.
Waalimu ni wanachama wa jamii ya kujifunza
Waalimu wa mfano mzuri huchangi katika kuendeleza shule kwa kufanya kazi kwa pamoja na wafanyakazi wengine katika sheria za ufundishaji, kuendeleza mitaala, kuwaendeleza wafanyakazi. Wanaweza kutathmini maendeleo na ugawaji wa vifaa kutokana na jinsi wanvyoeklewa malengo elimu na serikali kwa ujumla. Wanaelewa kuhusu shule maalum na vifaa vya jamii ambavyo vinaweza kutumika kwa faida ya wanafunzi, na wana ujuzi wa kutumia vifaa hivyo kama inavyohitajika. Waalimu waliofanikiwa hutafuta njia ya kufanya kazi kwa ushirikiano na ubunifu na wazazi, kuwatumia kwa uzalishaji katika mambo yafanywayo
shuleni.
National Board for Professional Teaching Standards. (1998).
Washington, DC:
Author. Available: http://www.nbpts.org
Vygotsky, L.S. (1978). Mind and
society: The development of higher